KARIBU KWENYE TOVUTI YETU YA
QFL MAGODORO DODOMA

Kununua godoro si sawa na kununua gari au koti. Godoro lako ni sehemu muhimu sana ya maisha yako. Mahusiano yako na Godoro unalolalia ni ya dhati na muhimu sana kwa kuwa yanachukua takribani theluthi moja ya maisha yako!
Kadri unavyolala salama na raha mustarehe ndivyo unavyo jihakikishia muenendo mzuri wa shughuli zako za mchana.
Godoro linaweza kuwa la ghali na pengine ndio bidhaa unayostahili kuifanyia utafiti wa kina kabla ya kafanya maamuzi ya kununua ili kujihakikishia afya njema na kujiepusha na usumbufu wa maradhi ya mgongo hapo baadae.
Kwa sababu hizi na nyingine nyingi, ni muhimu kuchukua muda na uvumilivu kuchunguza ni godoro lipi linakufaa kwa nyakati uliyopo ya Maisha yako.
QFL Magodoro tunakukaribisha kwetu ujionee godoro litakalokufaa na kukupa usingizi mwanana na kukuepusha na matatizo ya mgongo hapa mbeleni. Karibu.
Magodoro
QFL Ultra Inchi 12
Magodoro Dodoma
QFL Premier (PM) Inchi 10
Magodoro Dodoma
QFL Tape Edge Inchi 6 - 16
Magodoro Dodoma
QFL Orthopedic Inchi 6 na Inchi 8
Magodoro Dodoma
Quality Foam Limited
Quality Foam Ltd, Ni kampuni iliyoanzishwa mwaka 1992 kwa lengo la kuzalisha bidhaa za Magodoro. Kwa zaidi ya miongo miwili, Quality Foam Ltd imekuwa ikijishughulisha na utengenezaji wa Magodoro kwa njia za Kisasa.